Header Ads


ALICIA KEYS AMUHUSISHA DJ WA KENYA KATIKA WIMBO WAKE MPYA



DJ mmoja nchini Kenya amehusika katika kuzalisha mojawapo ya remix za wimbo '' In common'' wa mwanamuziki wa Marekani Alicia Keys.
Kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya,DJ Xpect ambaye jina lake ni Peter Kerre,aliorodheshwa na kampuni ya Sony Records na mwanamuziki huyo mwishoni mwa mwezi Juni.
DJ huyo mwenye makao yake huko Now York, Marekani aliwashinda wazalishaji wengine watatu baada ya kura iliofanywa katika mtandao wa Twitter kuwekwa na mumewe Alicia Keys Swizz Beatz mwishoni mwa wikendi akiwataka mashabiki kuipigia kura remix iliofanywa vizuri.
Miongoni ma DJ aliowashinda ili kupata fursa hiyo ni DJ wa Afrika Kusini Black Coffe ambaye alikuwa wa mwisho kujumuishwa katika waliotengeza remix ya wimbo huo.
Siku ya Ijumaa,Bi Keys alitoa remix hizo tatu ikiwemo ile inayomuhusisha Xpect na sasa inapatikana katika iTunes.

No comments

Powered by Blogger.