Header Ads


NEWSMEDIATZ: RAIS MAGUFULI "TBC MNASHINDWA KUENDANA NA WAKATI"


Magufuli amesema habari za TBC zinapaswa kutokubagua watu na Dini zao,Vyama wala Makabila yao kwani chombo hicho ndiyo msemaji mkuu wa Serikali.
Msemaji mkuu wa Serikali ni TBC1 na Redio ya Taifa, kazi yenu ni kutoa taarifa bila kubagua vyama vyao,bila kubagua dini zao, au makabila yao“Alisema Rais Magufuli.
Kwa upande mwingine Rais Magufuli amewasifia TBC kuwa wanajitahidi kutafuta  habari mpaka za vijijini ila tatizo lao kubwa ni kushindwa kuendana na wakati kwenye matangazo yao.
Mimi bahati nzuri ni shabiki mzuri sana wa TBC lakini problem yenu mnashindwa kuendana na wakati wa sasa“Alisema Rais Magufuli .
Rais Magufuli amefanya ziara ya kushitukiza katika Ofisi za TBC leo asubuhi na kuzungumza na uongozi wa TBC pamoja na kusikiliza kero za wafanyakazi.

No comments

Powered by Blogger.