KILO 48 ZA MADAWA YA KULEVYA ZATEKETEZWA TANGA
Mahakama kuu kanda ya Tanga imeteketeza dawa za kulevya aina ya ''heroin''kilogram 48.3 zilizokuwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 2.4 baada ya Mahakama hiyo kujiridhisha kutoka kwa mkemia wa serikali.
Dawa hizo zimeteketezwa katika tanuru la kiwanda cha kutengeneza
saruji cha Rhino kilichopo jijini Tanga chini ya ulinzi mkali wa polisi
na kushuhudiwa na wanasheria walikiongozwa na jaji wa Mahakama kuu kanda
ya Tanga mheshimiwa Upendo Msuya.
Akizungumza baada ya kuteketezwa kwa dawa hizo Mkurugenzi wa
mashtaka nchini (DPP) Biswalo maganga amesema dawa hizo zilikamatwa
Oktoba 09/2010 katika kizuizi cha Jeshi la Polisi kilichopo eneo la
Kabuku mkoani tanga yakitokea jijini Dar es Salaam yakiwahusisha raia
wawili watanzania Ismail Sheb Aslam na Rashid Said salim pamoja na raia
mmoja kutoka Iran Majid Ardmand ambao wote kwa pamoja wapo mahabusu huku
shauri lao likiendelea kusikilizwa.
Hili ni tukio la pili la kuteketezwa kwa shehena ya dawa za kulevya
aina ya heroin ambapo awali shauri kama hilo lilimhusisha Bakari Kileo
Bakari ambaye inadaiwa kuwa alikamatwa na kilo 90 za dawa za kulevya na
kutiwa hatiani na Mahakama kuu kanda ya Tanga kisha kuhukumiwa kwenda
jela miaka 25.
Post a Comment