MAHAKIMU KUPUNGUA MSONGAMANO WA KESI TANZANIA
Jaji mkuu wa Tanzania Othaman Chande amewataka mahakimu wa mahakama ambazo hazina msongamano wa mashtaka kupelekwa kwenye mahakama zenye mlundikano wa mashtaka ili kupunguza kero kwa watanzania ambao kesi zao zinachukua muda kusikilizwa kwa upungufu wa mahakimu.
Chande ameyasema hayo alipokuwa katika ziara yake mkoani Geita
yenye lengo la kutizama utendaji wa mahakama amesema kuna mahakama
zingine hazina mashauri mengi hivyo kukaa muda mrefu bila kufanya kazi
ambapo amewataka kwenda ambako kuna mashauri mengi kusaidia upatikanaji
wa haki.
Aidha amesema lengo la mahakama kwa mwaka huu wa 2016 ni
kuhakikisha mashauri yote yanasikilizwa na ifikapo mwisho wa mwaka huu
kuwa na kesi sifuri zinazosiamamiwa na mahakama zote.
Awali akimkaribisha jaji mkuu hakimu mkazi mwandamizi mfawidhi wa
mahakama ya wilaya ya Geita Ushindi Swallo amesema changamoto ya
miundombinu ya mahakama zilizonyingi wilayani hapa ndicho chanzo cha
ucheleweshwaji wa mashauri yaliyo mengi.


Post a Comment