PUNDA KUVALISHA NEPI KENYA
![]() |
| Mkokoteni wa punda |
Kaunti moja ya
Kaskazini mashariki mwa Kenya imechukua hatua zisizo za kawaida kulinda
barabara moja iliotiwa lami, kwa kuwavalisha nepi punda wanaotumia
barabara hiyo.
Mikokoteni yote inayofanya kazi Wajir sasa
italazimika kuweka begi nyuma ya wanyama hao ili kuokota kinyesi chao
kwa lengo la kuhakikisha barabara iko safi.Ni barabara kuu ya kwanza katika historia ya eneo hilo.Wakenya wameenda katika mitandao ya kijamii ili kusambaza uvumi vile punda wa Wajir wanapaswa kufuata sheria hiyo mpya mara moja.
Hii hapa taarifa iliotolewa na serikali ya eneo hilo:
''Tunashukuru mchango unaoletwa na waendesha mikokoteni ya punda kwa uchumi wa Wajir,hatahivyo,mji huo ni sharti usafishwe kila mara.Kutokana na hilo,mumeagizwa kusimamia kinyesi cha punda wenu ili kutochafua barabara.Hakuna Punda atakayeruhusiwa mjini bila mfuko wa kubebea kinyesi kufikia tarehe 29 mwezi Mei''.


Post a Comment