MAELFU YA WAHAMIAJI WAFURIKA ULAYA....
Maelfu ya watu wanazidi kuingia
barani ulaya kutoka nchini Eritrea kwa mwaka wa jana kuliko nchi
nyinginge zote za Africa na taarifa hii ni kwa muujibu wa takwimu za
umoja wa ulaya.
Nchi hii ndogo ya Eritrea, ambayo inakadiriwa kuwa
na watu wapatao milioni tatu unusu,ilijipatia uhuru wake kutoka kwa
Ethiopia miaka ishirini na tano iliyopita,baada ya miaka thelathini ya
vita.Kwa mujibu wa takwimu hizo, katika kipindi chote hicho hakukuwahi kufanyika uchaguzi, hakuna bunge, na hakuna uhuru wa vyombo vya habari.
Makundi ya kutetea haki za binaadamu yamekuwa yakiilaumu serikali kwa ukiukwaji wa haki za binaadamu, ikiwemo mateso, kifungo cha jumuiya, utumwa na kwa muda mrefu kulazimishwa kulitumikia jeshi.


Post a Comment