MAUAJI YA ALBINO SI TANZANIA TU MALAWI NAYO YAHOFIWA
Shirika la kutetea haki za
kibinadamu la Amnesty International, limeonya kutokea kwa wimbi jipya la
mauwaji dhidi ya Albino nchini Malawi.
Umoja wa mataifa
unakadiria kuwa visa 65 vya kutekwa kwa albino, kukatwakatwa viungo vyao
au kuuwawa, vimeripotiwa nchini humo tangu mwaka 2014.Amnesty, inasema kuwa watoto wa ulemavu wa ngozi, ndio walio kwenye hatari kubwa ya kuvamiwa au kutekwa nyara.
Watu hao wanawalenga, kwa sababu wachawi na madakatri wa kienyeji wanaamini kuwa sehemu ya viungo vya albino huleta baraka na utajiri iwapo vitatumika katika matambiko ya kitamaduni.
Amnesty inasema kuwa mashambulio dhidi yao yanaendelea licha ya serikali kupitisha sheria ya kuwapiga risasi wauwaji pindi wakipatikana kutekeleza uhalifu huo.


Post a Comment