PRITORIUS ANAUMWA HAWEZI KUTOA USHAHIDI
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius ambaye alitarajiwa kufikishwa kizimbani nchini Afrika Kusini kutokana na tuhuma za kumuua mpenzi wake hayuko katika hali nzuri kiakili kutoa ushahidi wake mahakamani.
Mtaalamu wa maradhi ya kiakili ameiambia mahakama kuwa Pistorius anaugua msongo wa mawazo na anawasiwasi mkubwa baada ya mahakama ya juu zaidi nchini humo kumuongezea makali ya makosa yake.
Mahakama hii ilikuwa imempata na hatia ya kuua bila kukusudia.

Hata hivyo mahakama ya juu zaidi iliamua kuwa mahakama hiyo ilikosea na hivyo mwanariadha huyo alistahili kujibu mashtaka ya mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp mnamo mwaka wa 2013.
Babake totoshoo huyo Barry leo anatarajiwa kutoa ushahidi wake baada ya kukosa kufanya hivyo katika kesi ya awali kutokana na kudhohofika kwa afya yake alipopata habari mwanawe alikuwa ameuawa kinyama.

Ikiwa mahakama itampata na hatia bwana huyo atafungwa jela miaka 15.
Hata hivyo muda halisi utaamuliwa na mahakama kwani tayari amekuwa akitumikia kifungo cha nyumbani.
Kauli ya mahakama hii inatarajiwa juma lijalo
Post a Comment