Header Ads


WAFUGAJI WATOA NG'OMBE 151 KUCHANGIA MADAWATI




Katika kuunga mkono agizo la Rais Magufuli la kila wilaya kutengeneza madawati katika shule zake,wafugaji katika wilaya ya Meatu wametoa Ng’ombe 151, Mbuzi 6 na Kondoo 3kwa ajili kuuzwa na fedha zitakazopatikana zitumike kutengenezea madawati.
Wakizungumza mara baada ya kukabidhi Ngo’mbe hao katika harambee ya uchangiaji wa madawati iliyofanyika wilayani Meatu ambayo imeitishwa na viongozi wa wilaya hiyo wafugaji hao wamesema wao kama wafugaji wako mstari wa mbele katika kuchangia shughuli za maendeleo isipokuwa kilio chao ni ukosefu wa maji,na malisho kwa ajili ya mifugo yao ambapo wameiomba serikali kuangalia kilio chao.
 
Ikiwapongeza wafugaji hao mkuu wa wilaya ya Meatu Erasto Sima amesema wilaya hiyo inatekeleza agizo hilo la Rais kwa kasi kubwa na kwamba hadi sasa wilaya wamefanikiwa kujitosheleza kwa viti na meza na kwamba hadi sasa wanaoupungufu wa madawati 7924.
 
Mbuge wa jimbo la Meatu Mh.Salimu Khamis amesema amepokea kilio cha wafugaji hao na kuwataka waondoe shaka kwani serikali itahakikisha wanapatiwa maeneo ya kuchungia ili mifugo yao isipate shida.
 
Katika harambee hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Mh. Jumanne Kishimba mbunge wa jimbo la Kahama jumla ya shilingi milion 550,890,324.ikiwa ni pamoja ahadi mbalimbali toka kwa wadau wa maendeleo ya wilaya hiyo zilipatikana.

No comments

Powered by Blogger.