Header Ads


MAMBA 100 WATOROKA HIFADHI KATIKA MAFURIKO



Mamlaka nchini Uchina inajaribu kutafuta takriban mamba 100 waliotoroka kutoka kwenye hifadhi moja baada ya mafuriko makubwa yanayoshuhudiwa nchini humo.


Mafuriko hayo yaliwawezesha mamba hao kuogelea na kuondoka kwenye eneo lilizingirwa kwenye hifadhi hiyo katika mkoa wa Anhui.


Ni nadra sana kupata Mamba hao wa Uchina mwituni.
Hata hivyo mamba huwindwa kutokana na ngozi yao inayouzwa kwa bei ghali mno pamoja na nyama yao na pia hutumika kuwaburudisha watalii.

Takriban watu 180 wamekufa maji kutokana na mafuriko hayo makubwa yanayoendelea kushuhudiwa nchini China.
Zaidi ya watu milioni moja wamelazimika kutorokea maeneo yenye milima ilikutoroka mafuriko yanayochacha.

No comments

Powered by Blogger.