VITU VITATU VILIVYOPIGWA MARUUFUKU NA PAUL MAKONDA KWENYE MKOA WA DAR
Ni July 2, 2016 ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepiga marufuku vitu vitatu kutoonekana katika mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye kongamano la Dini lililofanyika katika uwanja wa Taifa alisema..’Kwanza kwa watumiaji wa biashara ya Sheesha katika maeneo ya Bar, Clubs na sehemu zingine kuanzia leo ni marufuku katika maeneo hayo’- Paul Makonda
‘Pili ni marufuku kwa wavutaji wa Sigara kwenye sehemu za wazi kwani wataalamu wanasema ule moshi unamuathiri yule asiyetumia hiyo Sigara kuliko yule anayetumia Sigara’– Paul Makonda
‘Tatu ni marufuku kwa ushoga kwenye mkoa wangu wa Dar es Salaam na mashoga wote walio kwenye instagram na Facebook watakamatwa na wale wote wanao wa follow mashoga kwenye mitandao ya kijamii basi watakuwa na hatia ile kama ya mashoga‘- Paul Makonda
This type of message always inspiring and I prefer to read quality content, so happy to find good place to many here in the post, the writing is just great, thanks for the post.
ReplyDeletehttps://www.glentzes.gr/votanikos-mpouzoukia