KAMPUNI YA MAFUTA (SAHARA) YASIMAMISHWA KWA KUINGIZA MAFUTA YA NDEGE YALIYO CHAKACHULIWA
Serikali imeisimamisha kampuni ya
kimataifa ya Sahara kutojihusisha na zabuni za uingizaji mafuta yeyote
mbaka uchunguzi utakapokalimika baada ya kubaini imeingiza nchini maelfu
ya tani ya mafuta ya Ndege yaliyochanganywa na petroli na kuiamuru
kuingia gharama kusafisha matank ya mafuta na kuyaondoa mafuta hayo
nchini.
Maamuzi hayo ya serikali yametolewa baada ya waziri wenye dhamana
ya nishati na madini kutembelea maghara ya makampuni makubwa ya
usambazaji mafuta nchini na kusikia malalamiko ya uwepo wa mafuta
machafu ya Ndege yaliyongizwa nchini na kampuni hiyo na kusababisha
hasara kubwa.
Malalamiko hayo yalimfanya waziri wa mwenye dhamana ya nishati na
madini Profesa Sospeter Mhongo kutoa maamuzi ya serikali baada ya
kubaini ukweli kutoka kwa makampuni makubwa ya usambazaji ambayo yalidai
hayawezi kuyasambaza mafuta hayo ya Ndege na tayari yanamikataba na
mashirika mbalimbali ya Ndege.
Kutokana na maagizo hayo ya serikali Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
wakala wa serikali wa ununuzu wa mafuta kwa jumla-PBPA Bwana Michael
Mjinja alielezea namna ya mafuta hayo yatakavyoondolewa amesema tayari
muingizaji wa mafuta hayo ameingia nchini na kinachofanyika ni kuangalia
namna atakavyoyaondoa mafuta hayo.
Post a Comment