MAASAI WAMFANYIA IBADA RAISI MAGUFULI
Zaidi ya viongozi mia moja wa mila kutoka kabila la maasai kwenye wilaya za watu wa jamii hiyo wamekusanyika wilayani monduli kumisimika Kiongozi Mkuu wa mila wa koo ya Ilikisongo na kufanya ibada maalum ya kimila ya kumwomea Rais Magufuli na serikali yake waendelee kupambana na wafujaji wa mali ya umma.
Katika tukio ilo lililohudhuriwa na viongozi wa mila kutoka wilaya
za mikoa ya Arusha, Manyara, Morogoro na kwingineko pamoja baadhi ya
viongozi wa kisiasa ambapo wengi wao ni wa jamii hiyo viongozi wa mila
wamesema wapo tayari kushirikiana na serikali katika kuwafichua
watendaji wazembe na wauza ardhi ya umma ili kuwaondoa watanzania
kwenye dimbwi la umasikini.
Kiongozi aliyesimikwa kama mwenyekiti wa viongozi wa mila wa koo
hiyo Kibori Ngelipoi akizungumza huku akitafsiriwa kwakuwa hajui lugha
ya kiswahili amesema nafasi ya viongozi wa mila katika jamii ni kubwa
naye atahakikisha atatumia vizuri nafasi hiyo.
Baadhi ya viongozi wa kisiasa waliyo hudhuria tukio ilo wamewahasa
viongozi wa mila kutochanganya siasa na mila kwakuwa vitashusha ufanisi
wao katika kutatua masuala ya kijamii.
Post a Comment