Header Ads


MAGUFULI; MAOFISA WALA RUSHWA HADHARANI...

RAISI WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Rais John Magufuli amesema  maofisa wengi wa serikali wamekuwa  wakiwaomba rushwa  makandarasi  ili wawape zabuni  hivyo amewataka wawafichue  kwa  taasisi ya  kupambana na kuzuia rushwa nchini.
Mkuu huyo wa nchi ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa mkutano wa mwaka wa bodi ya makandarasi (CRB)
Kwa upande wake  Waziri wa ujenzi  uchukuzi mawasiliano  Profesa  Makame Mbarawa amesema  ni jukumu ya wakandasari  wa ndani kuhakisha wanalijenga Taifa lao.
 
Mwenyekiti wa bodi ya makandarasi (CRB), Consolata Ngimbwa, alimwomba Rais Magufuli kuweka mikakati ya kuwapa upendeleo makandarasi wazalendo.
 
Baadhi   ya  wakandarasi   walioshiriki   katika mkutano huo wamepongeza hatua za  Rais Magufuli za  kupambana  na  rushwa  na  kuahidi  kufanya kazi kwa uadilifu

No comments

Powered by Blogger.