Header Ads


TANGA MARUFUKU KUKARIBISHA WAGENI


Wakazi wa wilaya ya Kilindi kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za vitongoji na vijiji wameonywa kuacha kukaribisha wageni katika maeneo yao kwa sababu bado kuna viashiria vya kuwepo kwa vikundi vya uhalifu ambavyo viliwahi kuanzisha vikosi vya uhalifu vilivyodiriki kuua baadhi na askari huku mkuu wa kituo cha polisi akijeruhiwa vibaya kwa risasi.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara na wakazi wa kata ya Negero iliyopo wilayani Kilindi mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Kilindi Selemani Liwowa pamoja na watendaji wake wa serikali, wamesema hali ya kuwepo kwa vikundi hivyo vya uhalifu bado ipo kufuatia kukamatwa kwa baadhi ya watuhumiwa wanaojihusisha na kazi kutengeneza silaha za moto.
 
Hata hivyo baadhi ya raia wema waliounda vikosi vya kukabiliana na uhalifu waliofanikisha kuwakamata baadhi ya watuhumiwa wanaotengeneza silaha zinazotumika katika vitendo vya uhalifu, wameiomba serikali kupitia jeshi lake kuimarisha ulinzi kwa sababu baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa na silaha na nguo za jeshi la wananchi wameweka visasi kwa wananchi.
 
Kufuatia hatua hiyo, mkuu wa mkoa wa Tanga akizungumza na maafisa watendaji na wenyeviti wa serikali za mitaa jijini Tanga amewataka kuwafichua wageni wanaoingia katika maeneo yao na kwamba jeshi limeongeza nguvu katika zoezi la kukabiliana na wageni waliopo katika mapango ya Amboni ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya uhalifu.
 

No comments

Powered by Blogger.