MAN UNITED WAKUBALIANA NA MOURINHO
![]() |
Jose Mourinho |
Makubaliano ya
mkufunzi Jose Mourinho kuwa kocha wa kilabu ya Man United msimu ujao
yameafikiwa baada ya mazungumzo ya siku tatu.
Majadiliano kati ya
ajenti wa Mourinho Jorge Mendes na maafisa wakuu wa United yamekamilika
ijapokuwa hakuna kandarasi iliotiwa saini.Tangazo rasmi kutoka kwa klabu hiyo linatarajiwa siku ya Ijumaa.
Raia huyo wa Ureno atachukua mahala pake Louis van Gaal,ambaye alifutwa kazi siku ya Jumatatu, siku tatu baada ya United kushinda kombe la FA
Post a Comment