WANAFUNZI AMBAO HAWANA SIFA KUTIMULIWA VYUO VIKUU TANZANIA
![]() |
Tume ya vyuo vikuu nchini Tanzania |
Maelfu ya wanafunzi
wa vyuo na vyuo kikuu nchini Tanzania wako hatarini kufukuzwa katika
vyuo hivyo baada ya mamlaka kugundua kashfa kubwa inayohusisha usajili
wa wanafunzi ambao hawakufuzu.
Waziri wa elimu Joyce Ndalikacho
ametangaza kuvunjwa kwa bodi ya tume ya vyuo vikuu nchini humo na
kuwasimamisha kazi kwa mda maafisa kadhaa waandamizi.Magazeti ya the Guradian na Citizen nchini humo yanasema kuwa serikali imewafukuza wanafunzi 489 ambao walikuwa wamesajiliwa katika chuo kikuu cha St Joseph na kupewa mikopo ya serikali licha ya kuwa hawakufuzu kusomea ualimu.
Serikali imefunga chuo hicho kikuu kazkazini na kusini mwa Tanzania.
Post a Comment