MKWASA: MISRI KUTOISHIKA TAIFA STARS KWASASA....
Kocha
Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Charles Boniface Mkwasa amesema
kwamba mchezo ujao kati ya Mapharao wa Misri na Taifa Stars, utakuwa ni
fainali ya kuamua taifa litakalofuzu katika fainali za Kombe la Mataifa
ya Afrika AFCON hapo mwakani kutoka kundi G.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya mchezo kati ya Harambee Stars ya
Kenya na Taifa Stars ya Tanzania Mei 29, 2016, uliofanyika Uwanja wa Moi
Kasarani, Mkwasa maarufu kama Master anasema kwa msimamo na hali ilivyo
kwa sasa, “Najua Misri wanatufuatilia. Na hata Kenya kwa siku zote tatu
walikuwako. Najua Misri wanahitaji sare ili wafuzu kwa fainali hizi,
lakini hawataipata Tanzania.”
Mkwasa
anasema mchezo dhidi ya Misri, ana uhakika vijana wake watajitahidi ili
kupata matokeo mazuri baada ya Jumapili kufanya vema dhidi ya Harambee
Stars waliocheza mechi hiyo mbele ya mashabiki wao wachache ambao pia
hawakuchangamka kama wale wa Tanzania ambao licha ya kuwa ugenini
walichangamsha mji na uwanja.
Wakati
Misri wana pointi saba, Taifa Stars ina pointi moja na hivyo wa
kuibania au kupindua matokeo ya Misri isiende AFCON mwakani, basi ni
Tanzania hasa kama itawafunga Mapharao Jumamosi kabla ya kwenda Nigeria
Septemba, mwaka huu kucheza na Nigeria.
“Kama
nilivyosema, Misri wanakujawanahitaji pointi moja. Lakini sisi
tunahitaji pointi tatu. Mchezo wa leo unatosha kuona mapungufu
(upungufu). Maana ilikuwa mechi ngumu iliuyojaa nyota wote wa Kenya
ambao ni professionals, lakini mimi nilikuwa na local based players na
matokeo yamekuwa hayo.
“Tilianza
kufunga bao, lakini wakarudisha. Bora mchezo umeishia hivi maana najua
Wakenya hawana uvumilivu, tungewafunga hapa sijui kama tungetoka
salama,” amesema Mkwasa ambaye baadhi ya waandishi, hususani wale wa
Kenya walianguka kicheko kuashiria kuwa kuna matatizo katika utawala wa
soka.
Mkwasa
anasema ana taarifa namna ambavyo Misri wanaifuatilia Taifa Star
hususani ukusanyaji wa video kwa ajili ya kuona aina ya soka la
Tanzania, huku akisema: “Hawatafanikiwa kwa sababu soccer is the game of
different approach (Soka ni mchezo wenye mifumo tofauti). Hivyo
tulivyocheza na Kenya sivyo nitakavyocheza na Misri, nitakuwa na
approach yake.”
Anasema
ushindi wa Jumamosi ijayo ni wa kuvuna pointi tatu ili kupata kasi ya
kushinda mchezo dhidi ya Nigeria na kufungua ukurasa mpya wa Taifa Stars
kutengeneza mazingira mazuri ya kuwashinda Nigeria katika mchezo wa
mwisho hatua ya makundi utakaofanyika Septemba, mwaka huu.
“Tunaomba
Wakenya mtuombee. Nasi tunawaombea ili kama wote inatokea mwaka huu
tunakosa mafasi, basi iwe kheri kwa kipindi kijacho. Sisi tumekuja
kucheza kwenu katika mji wenu wenye baridi basi nanyi karibuni siku moja
dar es Salaam, Tanzania katika mji wetu wetu wenye joto, huenda
mkaambulia sare vile vile,” anasema.
Mkwasa
alipongeza Shirikisho la Soka Tanzania (FKF), kwa kuandaa mchezo huo
angalau kwa asilimia 70 kwa kushirikiana na Tanzania iliyojazia gharama
za juu sambamba vijana wake kwa kucheza kwa kujituma licha ya kuwakosa
nyota wake wa kulipwa na hivyo kupata picha na mbinu sahihi za kuivaa
Misri Jumamosi ijayo.
“Bado
tunaendele kujenga timu yetu, wengi ni vijana kama mlivyoona na wengine
ni mara ya kwanza wanacheza. Nimewapa nafasi na mmeona uwezo wao, bila
shaka tutafanya vema maana wengine ni under 21 wako kwenye kikosi. Huko
mbele tutakuwa na timu nzuri,” anasema Mkwasa akimtolea mfano Shiza
Ramadhani ambaye alipewa nafasi kwa mara ya kanza katika kikosi cha
kwanza akichukua winga ya kulia.

Post a Comment