KUCHAPWA VIBOKO 70 KWA ATAKAE HARIBU MAZINGIRA SIMANJIRO
Baada ya kukithiri kwa uharibifu wa mazingira kwenye mito na vyanzo vya maji uliyosababisha ukame katika kijiji cha Terati wilaya ya Simanjiro viongozi wa mila pamoja na serikali ya kijiji imeweka adhabu ya bakora sabini kwa mtu atakayeingiza mifugo kwenye maeneo hayo adhabu ambayo inasemekana imeanza kufakisha kukomesha tabia hiyo.
Wakizungumzia athari hizo baadhi ya viongozi wa mila na wakijamii
wamesema imesababishwa na uelewa mdogo wananchi juu ya umuhimu wa vyanzo
vya maji na tangu walipoanza kutoa adhabu ya kuchapwa bakora sabini kwa
anayekutwa ameingiza mifugo kwenye mto au chanzo cha maji mazingira
yameanza kurudi kwenye hali ya kawaida.
Mwenyekiti wa kijiji cha Terati Godson Nduya amekiri kuwa hali ya
uharibifu imekuwa mbaya ukame umekithiri na kuchangia kudumaza maendelea
ya jamii lakini mipango ya kunusuru inaendelea.


Post a Comment