Header Ads


RUSHWA YAMPONZA DAKTARI MTWARA


kassimu majaliwa waziri mkuu wa Tanzania
Waziri mkuu mh Kassimu Majaliwa amelazimika kutembelea hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ligula na kujionea madudu baada ya kuombwa na wananchi akiwa katika mkutano wa hadhara na kufanikiwa kumsimamisha kazi Dokta Fortunatus Namahala aliyeomba rushwa ya shilingi laki moja kutoka kwa mgonjwa.
Alipowasili katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ligula Mh Majaliwa akakumbana na kundi kubwa la wananchi na wakawa na haya ya kumueleza. 
 
Mh Majaliwa mara baada ya kutembelea hospitali hiyo na kupata malalamiko kutoka kwa wananchi akalazimika kuitisha kikao cha dharura cha madaktari pamoja na watendaji wa hosptali hiyo baada ya kuonyesha kukerwa na malalamiko ya wananchi dhidi ya madaktari.
 
Hata hivyo baada ya daktari aliyeomba rushwa kubainishwa na muhusika Mh waziri mkuu akawa na ujumbe huu. 
 
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Dokta Hindi Mastai akalazimika kumweleza waziri mkuu pamoja na lawama nyingi kwenda kwa madaktari mazingira wanayofanyia kazi ni haya.

No comments

Powered by Blogger.