MOTO WA TEKETEZA MALI ZA WANAFUNZI MBEYA
Moto mkubwa imeibuka katika shule ya
sekendari ya Iyunga ya jijini Mbeya na kuteketeza mabweni mawili na mali
zote za wanafunzi zilizokuwa ndani ya mabweni hayo.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 3:00 asubuhi wakati wanafunzi
hao wakiwa darasani, ambapo baadhi ya wanafunzi hao wanadai kuwa chanzo
cha moto huo ni hitlafu ya umeme ambayo imetokea ndani ya mabweni hayo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamesema kuwa moto huo
umeteketeza mali zao zote pamoja na vitanda vya kulalia, hivyo wakaiomba
serikali kuona uwezekano wa kuwasaidia namna watakavyoishi shuleni
hapo.
Afisa elimu wa mkoa wa Mbeya, Charles Mwakalila amesema kuwa katika
tukio hilo hakuna mwanafunzi ambaye amejeruhiwa wala kifo, na kwamba
athari za moto huo zimeanza kufanyiwa kazi.
Post a Comment