Header Ads


Watu 2 wamefariki na wengine kadhaa kunusurika baada ya mashua waliokuwa wakisafiria kuzama katika Ziwa Tanganyika.

Watu wawili wamekufa na wengine kadhaa wamenusurika baada ya mashua waliyokuwa wakisafiria kutoka  kijiji cha Kalya wilayani Uvinza  kwenda kigoma  mjini kukumbwa na dhoruba na kuzama katika Ziwa Tanganyika.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Ferdinand Mtui amesema mashua hiyo iliyokuwa na shehena ya mizigo na abiria sita ilikumbwa na dhoruba katika eneo la Msulumbuka katika pwani ya  milima ya hifadhi ya Taifa ya mahale .
 
Amesema dhoruba hiyo ilisababisha mashua inayoiwa Salum Line  kugonga mwamba na kupasuka hali iliyosababisha mizigo yote kuzama na watu wawili Pilila Ntagata na dada yake ambaye hajafahamika kufa huku wengine wakifanikiwa kuogelea mpaka nchi kavu.
 
Kutokana na hali hiyo ametoa tahadhari kwa wananchi hususan wavuvi na wanaoendesha shughuli za usafirishaji katika Ziwa Tanganyika kuzingatia utabiri wa hali ya hewa na kuchukua tahadhari za kiusalama .

No comments

Powered by Blogger.