Header Ads


Wavuvi zaidi ya 1000 wa kisiwa cha Kasarazi Mwaza wagoma kufanya kazi kupinga manyanyaso kutoka kwa wamiliki.

 Zaidi ya wavuvi 1,000 wa kisiwa cha Kasarazi wilaya ya Sengerema mkoani mwanza,wamegoma kufanya kazi kwa siku ya nne mfululizo wakipinga vitendo vya unyanyasaji,ikiwemo kunyimwa chakula  vinavyodaiwa kufanywa na wamiliki wa mitumbwi,huku uongozi wa serikali wilayani humo ukilalamikiwa kwa kufumbia macho vitendo hivyo vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Katibu wa umoja huo wa wavuvi wapatao 1,165 waliopo katika kisiwa cha Kasarazi halmashauri ya wilaya ya Buchosa Boniphace Mgeta amesema wameamua kugoma kuingia ziwani kuendelea na shughuli zao za uvuvi kwa madai ya kunyanyaswa na matajiri hao,huku mkuu wa wilaya hiyo Zainab Talack akishindwa kuupatia ufumbuzi mgogoro huo licha ya kukutana na pande hizo mbili ofisini kwake .
 
Uongozi wa wamiliki wa vyombo vya uvuvi wa kisiwa hicho cha Kasarazi kilichomo ndani ya Ziwa Victoria, kupitia kwa katibu wao Msilikale Juma amesema chanzo cha mgogoro huo ulioanza kufukuta kuazia mwezi Aprili mwaka huu ni hujuma inayodaiwa kufanywa na baadhi ya wavuvi wasio waaminifu na kusababisha hasara ya mamilioni ya shilingi kwa wamiliki wa vyombo vya uvuvi.
 
Mkuu wa wilaya ya Sengerema Zainab talack akizungumza na ITV kwa njia ya simu kutokea wilayani Sengerema amekiri kuutambua mgogoro na kuzitaka pande zote mbili kukaa chini na kufanya mazungumzo yenye lengo la kufikia mwafaka.
 

No comments

Powered by Blogger.