KILIO CHA HAJI SUNDAY MANARA KWA MUHAMMAD ALI HIKI HAPA
Tuite
nini fazaa? Taharuki? Nadhani tuliite pigo la ulimwengu. Sshujaa wa
watu wote na mfalme mwema Muhammad Ali ametutoka ghafla leo huko
Scottsdale Arizona leo tarehe 4 June 2016.
Nimeita
pigo kwa sababu king Ali alikuwa ni alama ya ustaarabu mpya duniani.
Ustaraabu wa kuwatambua watu wa imani tofauti na wakaheshimiana,
ustaraabu wa thamani ya mtu mweusi, ustaraabu wa kutumia sanaa ya
michezo hususan fight. Kuwa ni kielelezo cha upendo, amani na
mshikamano.
Najua
washangaa kwa nini nimeanza na falsafa hizo ninazo sababu lakini
niitaja kubwa moja huwa kila siku nasema michezo inaweza kuinganisha
jamii iliyotengana. Michezo inaweza kuleta maji penye kiu michezo
inaweza kuleta tiba penye maradhi, michezo inaweza kuleta amani penye
vita na ndiyo maana king mwingine duniani Pele aliweza kusimamisha vita
ya Biafra kule Nigeria. Pale klabu yake ya Santos ilipotembelea taifa
hilo miaka ambayo vita ilikuwa ikipiganwa.
Ali
ameleta kila kitu kupitia ngumi kaleta maji penye kiu kule Afghanistan.
Kaleta amani penye vita kule Iraq na hata tiba penye maradhi kule
Ethiopia 1983.
Ni nani king Ali?
Ni
mfalme wa mchezo wa ngumi duniani ambaye hajapata kutokea ni mwanamiche
muungwana zaid duniani kuwahi kutokea lakini ndio mwanamichezo bora wa
karne iliopita akipambana mapambano 61 ya ngumi.akishinda 56 huku 37
akishinda kwa KO. Licha ya hayo king Ali ni mshindi wa medali ya dhahabu
ya olimpiki kule Rome itali 1960, zama hzo akifight na uzito wa light
heavy kabla ya kujiunga na ngumi za kulipwa ambako alipigana katika
uzito wa heavyweight .
Bahati
mbaya hii makala hii nilipanga iwe fupi ningekupa habari za mapambano
yake maarufu hususan na Joe freizer na George foreman. Ila tambua dunia
leo imempoteza shujaa wa watu wengi kama si wote.
Kuna
wakati mzaliwa huyo wa Louisville Kentucky ambae alipewa jina la
Cassius Marcellus Clay Jr na baadaye kusilimu kisha kutumia jina lake
maaruf Muhammad Ali. Alipata kumdhalilisha kwenye ring bingwa wa zamani
Liston kwa kumlazimisha amwite jina lake jipya Muhammad.
Liston
alikuwa hatambui imani mpya ya Alli. Na king akaamua kumlazimisha
kumwita jina jipya ulingoni.....who's my name? Ali alisikika akimuuliza
Liston ulingoni huku akitupa jeb jeb..liston hatimaye alilitamka jina
hilo Ali.
Miaka yake 74 ulimwenguni ameacha alama kubwa sana na dunia haitamsahau kiumbe huyo aliyejaaliwa sura za kina nabii Yusuf.
Mungu mpokee people's champion Louisville RIP king of the kings....man of the century....
Nimehemewa na kuandika..chozi langu hili linanikumbusha msiba wa madiba...
Inna lillah wa inna ilaihi raajiun
Post a Comment