Header Ads


WAFANYA KAZI WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI WAASWA KUWAJIBIKA ILI KUONGEZA KASI YA MAFANIKIO




Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One JOYCE MHAVILLE ametoa changamoto kwa wafanyakazi wa vyombo hvyo vya utangazaji kuwajibika kwa nafasi zao katika kuendeleza kasi ya mafanikio ya kampuni hiyo.
Amesema mafanikio ya sasa ya kampuni hiyo yametokana na juhudi za wafanyakazi wake na kwamba katika kipindi hiki cha ushindani wa vyombo vya utangazaji juhudi za ziada zilikuwa zinahitajika katika kuleta ufanisi na kutafuta matangazo ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha mapato yake.
Bi JOYCE MHAVILLE alikuwa akizungumza kwenye sherehe ya mwaka kwa ajili ya wafanyakazi wa ITV/Radio One pamoja na baadhi ya wawakilishi wake wa mikoani na Visiwani.
Kwa kawaida baadhi ya wageni mashuhuri kualikwa kujumuika na wafanyakazi wa ITV/Radio One na mwaka huu mwanamuziki ALI KIBA na mwigizaji wa tathmiliya ya ISIDINGO SISA HEWANA MAARUFU KAMA SKUMBUZO walikuwa miongoni mwa wageni hao.
Katika hatua nyingine Mwanahabari na Mtangazaji mkongwe Raifred Masako wa ITV/Radio One ambaye ameamua kustaafu Kufanyakazi na ITV/Radio One akapata fursa kuwaaga waliokua wafanyakazi wenzake na kuwapa siri ya mafanikio katika kufanya kazi na watu.

No comments

Powered by Blogger.