Header Ads


NJAA INAWAKABILI RAIA WA SYRIA



Umoja wa mataifa umearifu kwamba raia wa Syria wapatao sitini na wawili wamekwama katika miji minne tofauti na wako katika hatari ya kufa kwa njaa.
Muwakilishi mkazi wa umoja wa mataifa aliyeko mjini Damascus, Yacoub El Hillo, ametoa tamko la kuhitaji msaada wa dharula hasa upande wa dawa na kuwahamisha wagonjwa na kuwapeleka katika maeneo yenye tiba thabiti ikiwamo msaada wa haraka na huduma thabiti za mahitaji ya kibinaadamu.
Kumekuwa na huduma endelevu kwa wanawake wanaojifungua katika miji ya Madaya na Zabadani, taarifa zinaeleza kwamba miji miwili iliyoko pembezoni mwa mji mkuu inadhibitiwa na vikosi vinavyoitii serikali.
Raia wamekuwa wakizingirwa na waasi hasa katika miji iliyoko upande wa Kaskazini-Magharibi mwa miji ya Foua na Kafraya inakabiliwa na hali zinazoshabihiana kuwa chini ya udhibiti wa waasi.

No comments

Powered by Blogger.