Donald Trump amewalaumu waandishi wa
habari baada yake kushutumiwa kwa matamshi yake ambapo alidaiwa
kuwahimiza wafuasi wake wamuue mpinzani wake Hillary Clinton wa chama
cha Democratic.
Alikuwa amewaambia wafuasi wake kuwa wanaweza kumzuia hasimu wake Bi Clinton kwa kutekeleza haki zao za silaha.
Alisema
Bi Clinton anaweza kupeleka haki zake huria za kisheria mbele ya
Mahakama ya Juu kama atashinda urais mwezi Novemba, na kufuta haki ya
raia kumiliki silaha.
Akihutubia mkutano wa kisiasa katika jimbo
la North Carolina, Bw Trump alidokeza kuwa haki za umiliki wa silaha
zinaweza kusaidia kumzuia Bi Clinton kuchukua mamlaka.
Kauli yake hiyo imezua hasira kwenye mitandao ya kijamii, wengi wakimshutumu kwa kuchochea ghasia.
Lakini
muda mfupi baadaye alijitetea na kusema kuwa alikuwa tu anawataka
wanaounga mkono haki za umiliki wa silaha kupiga kura kwa wingi.
Baadaye
alisema wanahabari wa shirika la habari la Fox News walipinda matamshi
yake na kuyafanya yaonekane kana kwamba alikuwa anawahimiza wafuasi wake
wenye silaha wazitumie kumuangamiza Bi Clinton.
Hii si mara ya kwanza kwa Bw Trump kulazimika kukosoa kauli zake.
1. Kumbeza mlemavu
Aliwahi
kukanusha kumbeza mwandishi wa habari mlemavu wa gazeti la New York
Times Bw Trump alilegeza mikono yake alipokua akielezea makala kuhusu
mashambulizi ya 9/11 iliyoandikwa na Serge Kovaleski, ambae ana ulemavu
wa mikono. Hata hivyo mwanasiasa huyo alisistiza kuwa hakujua ripota
huyo anafanana vipi na kwamba anawaheshimu watu wenye ulemavu.
2. Iran kulipwa pesa
Donald
Trump aliwahi kufafanua baada ya awali kudai kuwa aliona mkanda wa
video wa malipo ya pesa ya Marekani kwa Iran. Alitoa madai hayo kwenye
mkutano wa kisiasa. Trump alisema malipo yalikua na uhusiano na Iran
kukubali mapatano ya nyuklia
3. Wanawake kutoa mimba
Donald
Trump alifuta kauli yake ya awali ambapo alisema wanawake waliotoa
mimba waadhibiwe saa chache tu baada ya kutoa pendekezo hilo.
Alipendekeza kuwa "aina fulani ya adhabu " itolewe kwa wanawake waliotoa
mimba kama zitakuwa kinyume cha sheria. Lakini baada ya ukosoaji mkubwa
, Bw Trump akarejelea msimamo wa chama cha Republican kwamba mtu
anaefanya kitendo cha utoaji mimba anapaswa kuadhibiwa, si mwanamke
pekee.
4. Kudukuliwa kwa Clinton
Donald
Trump alisema alitumia tu lugha ya mzaha alipokowaalika warusi wadukue
jumbe za Bi Hillary Clinton zilizopotea. Aliikiambia kituo cha
televisheni cha Fox News kwamba chama cha Democrat kilikua tu kinatumia
mzozo huo kukwepa masuala makuu. Kauli zake zilikua kuhusu jumbe 30,000
za barua pepe za Bi Clinton ambazo hakuziwasilisha kama sehemu ya
uchunguzi kuhusu jumbe za siri. "nilikua najaribu kuwa mzushi tu," Bw
Trump alikiambia kituo cha Fox News.
Post a Comment