Header Ads


WANAFUNZI 36 WAPATA UJAUZITO SHINYANGA


Wanafunzi wakike 36 wa shule za sekondari katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wamebainika kupewa ujauzito na kulazimika kukatisha masomo yao huku baadhi ya watendaji wa serikali wakitajwa kuhusika kuwapa ujauzito wanafunzi hao.
Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wamedai kuwa ongezeko la mimba kwa wanafunzi limekuwa kikwazo cha maendeleo ya elimu kwa watoto wakike huku wakimtaka mkuu wa wilaya hiyo Bi.Hawa Ng’humbi kufuatilia na kutoa adhabu kali kwa watumishi wa serikali pamoja na waendesha bodaboda ambao wanatuhumiwa kushiriki kuwapa mimba wanafunzi hao.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Bw.Boniface Butondo amesema serikali haiwezi kuvumilia na kufumbia macho mchezo huo mchafu unaofanywa na baadhi ya watumishi wa serikali huku mkuu wa wilaya ya Kishapu Bi.Hawa Ng’umbi akidai kuwa zoezi la kubaini watu hao limeanza rasmi na wazazi watakaoficha ukweli kuhusu jambo hilo pia watachukuliwa hatua za kisheria.

No comments

Powered by Blogger.